1
Faculty of Education Tom Mboya University College, A constituent College of Maseno University, Kisumu, Kenya P.O. Box 199-40300
Abstract
Malengo ya Makala hii yalikuwa ni kuchanganua miktadha mbalimbali ambapo utanzu wa muziki wa Taarab ya Mipasho umeingiliana na utanzu wa Ushairi Simulizi, Majigambo. Makala hii iliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini iliyoasisiwa na Julia Kristeva (1960) baada ya kuizua kutokana na nadharia ya Mikhail Bakhtin ya Usemezano ambapo imetumika kushughulikia mwingiliano tanzu katika Taarab-Mipasho. Pia nadharia hii imetumika katika kufafanulia uhuru na ubunifu wa mtunzi wa kuingiza vipengele vipya katika kazi. Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Ukusanyaji data ulihusisha usikilizaji, utazamaji na unukuzi daftarini wa nyimbo za Taarab ya Mipasho ili kupata mistari, vifungu vya maneno na stanza zilizobainisha mwingiliano tanzu. Sampuli ya utafiti ilikuwa nyimbo 6 za muziki wa Taarab ya Mipasho ambazo ziliteuliwa kumaksudi. Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulitolewa kwa njia ya maelezo ya kina yaliyohusisha udondoaji na ufafanuzi wa mistari, vifungu vya maneno na stanza zenye kudhihirisha mwingiliano tanzu kutoka kwa data asili. Kutokana na matokeo ya utafiti, mwingilianotanzu mkubwa ulibainika katika uwasilishaji wa muziki wa Modern Taarab ya Mipasho uliorejelewa. Utafiti huu unawachochea wahahakiki wengine wa fasihi simulizi katika kufanya uchunguzi zaidi katika mitindo mingine ya nyimbo za modern taarab kwa misingi ya nadharia mbalimbali za fasihi.
License
Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
Mwingiliano WA Utanzu WA Modern Taarabu- Mipasho Na Ushairi Simulizi, Majigambo © 2026 by Jackline Njeri Murimi licensed under CC BY-NC-ND 4.0
All papers should be submitted electronically. All submitted manuscripts must be original work that is not under submission at another journal or under consideration for publication in another form, such as a monograph or chapter of a book. Authors of submitted papers are obligated not to submit their paper for publication elsewhere until an editorial decision is rendered on their submission. Further, authors of accepted papers are prohibited from publishing the results in other publications that appear before the paper is published in the Journal unless they receive approval for doing so from the Editor-In-Chief.
Himalayan Journal of Education and Literature open access articles are licensed under a Creative Commons Attribution-Share A like 4.0 International License. This license lets the audience to give appropriate credit, provide a link to the license, and indicate if changes were made and if they remix, transform, or build upon the material, they must distribute contributions under the same license as the original.